Vigezo vya Timu Kushiriki Kombe la Shirikisho
Ili timu ishikilie nafasi ya kushiriki kwenye CAF Kombe la Shirikisho, kuna vigezo kadhaa ambavyo hutumika, ikiwa ni pamoja na:
- Ubingwa wa Kombe la FA – Timu zinazoshinda makombe ya ndani ya nchi zao (FA Cup) hupata nafasi ya moja kwa moja kushiriki.
- Kutolewa Katika Raundi za Awali za Ligi ya Mabingwa ya CAF – Timu zinazoshindwa kufuzu kwenye Ligi ya Mabingwa za CAF mara nyingi hupata nafasi ya kushiriki kwenye Kombe la Shirikisho kama njia mbadala.
- Msimamo wa Ligi za Ndani – Timu zinazomaliza katika nafasi za juu kwenye ligi kuu za nchi zao, lakini hazikufuzu kwenye Ligi ya Mabingwa, zinaweza kupata tiketi ya kushiriki.
Timu Zilizofuzu Makundi CAF Kombe la Shirikisho 2024/2025
Kwa msimu wa 2024/2025, timu zifuatazo zimefanikiwa kufuzu hatua ya makundi ya CAF Kombe la Shirikisho:
Nafasi |
Timu |
Nchi |
1 |
Stade Malien |
Mali |
2 |
Zamalek SC |
Misri |
3 |
RS Berkane |
Morocco |
4 |
CD Lunda Sul |
Angola |
5 |
CS Sfaxien |
Tunisia |
6 |
Constantine |
Algeria |
7 |
Simba SC |
Tanzania |
8 |
Orapa United |
Botswana |
9 |
Bravos do Maquis |
Angola |
10 |
Stellenbosch |
Afrika Kusini |
11 |
Black Bulls |
Msumbiji |
12 |
Enyimba FC |
Nigeria |
13 |
ASEC Mimosas |
Ivory Coast |
14 |
Al Masry |
Misri |
15 |
ASC Jaraaf |
Senegal |
16 |
USM Alger |
Algeria |
Vilabu hivi vina historia ya kutawala mashindano ya ndani na nje ya nchi zao, na hivyo kufanya michuano ya mwaka huu kuwa ya kusisimua zaidi.
Timu kama Simba SC kutoka Tanzania na Zamalek SC kutoka Misri ni miongoni mwa vilabu vyenye mashabiki wengi, na itakuwa ya kuvutia kuona jinsi wanavyopambana na timu kutoka nchi tofauti barani Afrika.
Mashindano ya CAF Kombe la Shirikisho 2024/2025 yanatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa, huku timu zilizofuzu zikiwa zimejipanga vizuri. Kwa updates zaidi za mashindano na timu hizi, hakikisha unatembelea nectapoto.com, blogu bora kwa habari za michezo na updates nyingine za soka barani Afrika.