JIUNGE NA GROUP LA AJIRA TANZANIA
MICHEZO

Dirisha Dogo Tanzania Bara 2024/2025: Tetesi na Madai ya Usajili

Dirisha Dogo Tanzania Bara 2024/2025: Tetesi na Madai ya Usajili

Dirisha dogo la usajili kwa msimu wa 2024/2025 Tanzania Bara linakaribia kufunguliwa rasmi tarehe 15 Desemba 2024. Hii ni fursa muhimu kwa vilabu vya Ligi Kuu Tanzania Bara kurekebisha vikosi vyao kwa ajili ya kuimarisha ushindani katika hatua za mwisho za msimu. Kutokana na ushindani mkali unaoshuhudiwa, tetesi za usajili zimeanza kushika kasi, huku wachezaji na makocha mbalimbali wakihusishwa na vilabu tofauti.

Usajili wa wachezaji katika dirisha dogo hutoa nafasi kwa vilabu kurekebisha mapungufu yaliyobainika kwenye kikosi katika nusu ya kwanza ya msimu. Vilabu huongeza nguvu mpya, kurekebisha sehemu dhaifu, na kuimarisha safu zao kwa lengo la kufanikisha malengo yao, iwe ni kushinda taji, kubaki ligi kuu, au kupata nafasi za kimataifa.

Kwa mfano, Young Africans na Simba SC zimekuwa zikihusishwa na wachezaji mbalimbali, zikiashiria nia yao ya kuongeza nguvu kwenye vikosi vyao. Dirisha dogo pia ni muhimu kwa wachezaji wanaotafuta nafasi za kucheza, hasa wale ambao hawajapata muda wa kutosha wa kucheza katika vilabu vyao vya sasa.

Tetesi za Usajili Dirisha Dogo Tanzania Bara 2024/2025

Young Africans (Yanga SC)

  1. Kelvin Nashon (Kiungo Mkabaji) – Inaripotiwa kuwa Yanga wanamtaka Kelvin Nashon ili kuongeza nguvu eneo la kiungo mkabaji.
  2. Harvey Onoya (Kiungo raia wa DRC) – Yanga wanatafuta saini yake ili kuimarisha safu ya kiungo.
  3. Fredy Michael Koublan – Yanga pia wanapanga kumsajili mchezaji huyu.
  4. Jonathan Ikangalombo (Winga wa AS Vita) – Anatajwa kama lengo la Yanga kuongeza kasi ya kushambulia.
  5. Fahad Bayo (Striker wa Uganda) – Baada ya kuachana na timu yake, Yanga wanatafuta saini yake.
  6. Jonathan Sowah – Singida Black Stars wanapanga kumtoa kwa Yanga huku Kennedy Musonda akipelekwa kwa mkopo.

Simba SC

  1. Foday Trawally (Kiungo Mshambuliaji) – Anatajwa kuwa njiani kuondoka Simba.
  2. Abdelhay Forsy – Simba wanapanga kumsajili beki huyu ili kuimarisha safu ya ulinzi.
  3. Sabri Kondo, Charles Senfuko, na Ibrahima Seck – Wote wanahusishwa na Simba katika dirisha hili dogo.
  4. Kambou Dramane – Simba na Yanga wanapambana kupata huduma ya mchezaji huyu.
  5. Ayoub Lakred – Simba inakabiliwa na uwezekano wa kumuachia mchezaji huyu huku akihusishwa na Raja Casablanca na JS Kabylie.

Singida Black Stars

  1. Larry Bwalya – Anawindwa na Singida Black Stars pamoja na Pamba Jiji.
  2. Bruno Gomez (Kiungo Mbrazil) – Anaweza kurejea Singida Black Stars.
  3. Jonathan Sowah – Tayari amesajiliwa na Singida Black Stars lakini kuna mpango wa kubadilishana wachezaji na Yanga.

Azam FC

  1. Salim Mwalimu – Anahitajika na Azam FC ili kuimarisha safu yao.
  2. Lasinne Kouma – Azam wanapambana na Simba na Yanga kupata saini ya kiungo huyu.

Wachezaji Wanaohusishwa na Vilabu Zaidi ya Kimoja

  1. Lameck Elias Lawi (Beki) – Simba, Yanga, na Azam wanamfukuzia. Anaweza kusajiliwa dirisha dogo au kubwa.
  2. Mamadou Koita (Kiungo wa Mali) – Yanga wanamfukuzia, huku akitajwa kama kiungo mwenye uwezo mkubwa.
  3. Kibwana Shomary (Beki) – Anatakiwa KMC kwa mkopo.

Mabadiliko ya Makocha na Uongozi

Tetesi zinaonyesha kuwa Yanga inaweza kufanya mabadiliko makubwa kwenye benchi la ufundi. Kocha mkuu Miguel Gamond pamoja na msaidizi wake wanahusishwa na nafasi katika JS Kabylie ya Algeria, huku Abdelhamid Moalin akitajwa kuwa kocha msaidizi mpya wa Yanga.

Kwa upande mwingine, masuala ya kiutawala pia yameibuka. CEO wa Yanga, Andre Mtine, na mwanasheria Simon Patrick wamekalia kuti kavu, hali inayoashiria uwezekano wa mabadiliko makubwa katika uongozi.

Dirisha dogo la usajili ni kipindi chenye msisimko mkubwa, si tu kwa vilabu bali pia kwa mashabiki wanaosubiri kuona wachezaji wapya watakaojiunga na timu zao. Mabadiliko yanayotarajiwa msimu huu yanaweza kuathiri kwa kiasi kikubwa mwenendo wa ligi katika nusu ya pili ya msimu wa 2024/2025. Mashabiki wanapaswa kufuatilia kwa karibu, kwani tetesi nyingi huenda zikawa kweli wakati dirisha dogo litakapofunguliwa rasmi.

About the author

admin

Leave a Comment

JIUNGE NA GROUP LA AJIRA TANZANIA