Orodha ya Wachezaji Wote Walioshinda Tuzo za TFF 2023/24
Sherehe za ugawaji wa tuzo kwa wachezaji waliofanya vyema katika msimu wa 2023/2024, maarufu kama TFF Awards, zilifanyika katika ukumbi wa Super Dome. Usiku wa tarehe 1 Agosti 2024, jijini Dar Es Salaam, lilifanyika tukio kubwa la kimichezo nchini Tanzania.
Katika usiku huo wa ugawaji wa tuzo, wachezaji mbalimbali walipata tuzo zao kwa kutambua juhudi zao walizozifanya msimu huu. Sokoleo.co.tz imekuwekea orodha ya wachezaji wote na tuzo walizoshinda. Endelea kutembelea tovuti yetu kwa habari mbalimbali za kimichezo, au pakua app yetu hapo chini.
Mfungaji Bora wa Ligi
Kwa msimu wa 2023/24, Stephanie Aziz Ki, kiungo mshambuliaji wa klabu ya Yanga SC, ametangazwa kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania.
Golikipa Bora, Kombe la Shirikisho (CRDB)
Mlinda mlango wa klabu ya Yanga SC, Djigui Diarra, ameshinda tuzo ya golikipa bora wa Michuano ya FA (CRDB FEDERATION CUP), akiwashinda Khomein Abubakar wa Ihefu (Singida Black Stars) na Mohamed Mustafa wa Azam FC.
Golikipa Bora, Ligi Kuu Bara
Ley Matampi ameshinda tuzo ya golikipa bora wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kwa msimu wa 2023/2024, akiwashinda Djigui Diarra wa Yanga na Ayoub Lakred wa Simba SC, mlinda mlango wa Coastal Union.
Beki Bora Ligi Kuu Bara
Ibrahim Bacca, beki wa Yanga SC na Timu ya Taifa ya Tanzania, ameshinda tuzo ya beki bora wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara msimu wa 2023/24.
Kiungo Bora
Stephanie Aziz Ki, kiungo mshambuliaji wa Yanga SC kutoka Burkina Faso, ameshinda tuzo ya kiungo bora wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2023/24, akiwashinda Kipre Junior wa Azam FC na Feisal Salum ‘Feitoto’ wa Azam FC.
Mchezaji Bora wa Tanzania, Anayecheza Nje
Mbwana Samatta, nahodha na mshambuliaji wa klabu ya PAOK ya Ugiriki, ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa kiume wa Tanzania anayecheza nje ya Tanzania.
Mchezaji Bora (MVP) Kombe la Shirikisho
Faisal Salum ‘Feitoto’ wa Azam FC ameshinda tuzo ya mchezaji bora (MVP) wa Kombe la Shirikisho la CRDB (CRDB Federation Cup) kwa msimu wa 2023/24.
Mchezaji Bora Ligi Kuu ya Wanawake (TWPL) – Aisha Mnunka
Mfungaji Bora Ligi ya Wanawake – Aisha Mnunka
Kipa Bora Ligi ya Wanawake – Caroline Rufo